|
By... Mwl. Julius Kambarage Nyerere |
|
Ikulu ni mahali patakatifu, ikulu ni mahala patakatifu |
|
Mimi sikucha guliwa na wananchi wa Tanzania |
|
Kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi |
|
Claps claps claps |
|
By... Roma |
|
Drop drop drop drop drop yop |
|
Haaa haaa... yes Surprise ...Tongwe records |
|
We are here for revolution wooord |
|
Mr. president .welcome to white house |
|
Thank you... aaaah ...thank you ...yeaaah |
|
Mi ndo' roma mkatoliki mwenye asili ya kiyahudi |
|
Mpare wa milimani sa lamu ya kikwetu urewedi |
|
We ni mkwere wa chalinze ambaye hutamsahau mnyakyusa...(Mwakyembeee) |
|
Aliye wafundisha monduli siasa |
|
Aliyekula kiapo kwa agano jipya la wakorintho |
|
Siyo msabato mwenye siasa za kubattle kama Zitto |
|
Mwenye wito wa Appocalypto husssle za Kambikatoto |
|
Msaka ndoto kama kristo shujaa kama Mrisho Mpoto |
|
Jasiri kama Mandela busara kama Nyerere |
|
Niliyejificha mapangoni mithili ya Otango Osale |
|
So usinidanganye kwa uchawi waaa kutumia ndulele |
|
Au vita vya majimaji nife kama Kinjekitile |
|
Hatutaki siasa za kale, siku hizi tunawahi kubalehe |
|
Nawapa pole wakazi wote wa Tandale kwa Mtogole |
|
Akhsante Sheikh umeniita ikulu sio kisa nina nyota ya mshale |
|
Najua mvi sio busara ila naomba amani itawale |
|
Ikulu yako ina thamani zaidi ya falme za kiarabu |
|
Cha ajabu hawaithamini na inapoteza thawabu |
|
Taifa lilikutabri tangu enzi ukiwa waziri |
|
J.K wa 2 utakuja ongoza hii serikali |
|
Yenye vilio kote kama kina mama wa Galilaya |
|
Wanaoutafuta ukombozi wasimamishe Pobilahaya |
|
Viongozi wetu ni mafia na mabeautifull lier |
|
Nilikuwa na ndoto hizo ila bado hawaja niinspire |
|
Angalau mapinduzi kama Macio Maximo |
|
Usihangaike kumtafuta Roma... mi!! Hakimu wa getho |
|
Mwenye sauti ya mamlaka!!! iliyomfikisha Mrombo Keko |
|
Baada ya kukemea ufisadi na sera za Karamagi |
|
Na waliokula jasho letu kwenye migodi ya Buzwagi |
|
Utazuia vipi ongezeko la wimbi la ukeketaji... |
|
Wakati Ngariba ndo' diwani wa kata kwenye kijiji!! |
|
Neither do I...!! hongera ulipima ukimwi |
|
Watanzania nasi tuamke tusimpige kibao tu Mwinyi |
|
Hapa nagundua aya-tul - munafik - thalatha |
|
Inawezekana aliishia alifu wakati anasoma madrasa |
|
Huu sio muda wa kujadili kesi za Manji na Mengi |
|
Hayo ya Mungu we Kaisari jadili mambo ya msingi |
|
Teacher alipojiita mtabiri Tanganyika wote vipofu |
|
Padre wa kwanza pentekoste ubatizo wa maji marefu |
|
Machozi yalinitoka Segera watoto hawapati haki |
|
Wengi wamekimbia shule basi lije wauze visheti |
|
Wanaosomeshwa kwa mtaji wa chapati na uvuvi wa samaki |
|
Wabunge wao wamekaa na wanajiita wanaharakati!! |
|
Rudi kwenu kahamasishe nduguzo hawana taaluma |
|
Wazaramo wamegoma soma still mwali wanamcheza ngoma |
|
Wanalia Kilwa Kivinje huku wanaocheka ni wabunge |
|
Walionunua kura ya bibi kwa kumuhonga doti ya kitenge |
|
Hata wamasai walikuchagua kwa kura nyingi za upendo |
|
Wakiamini mtetezi yuaja wa jimbo la Oldoyo Sambo |
|
Waambie what is going on ndani ya himaya ya bwawa la Mtera |
|
Waonyeshe na mikataba ya utawala wa mgodi wa Kiwira |
|
Jeshi lote kwenda Tarime hawakuwa na njia mbadala |
|
Na walioteketea Mbagala!! |
|
Mr.pres ... Haya masikharaaaa!!! |
|
Sina maana utoke wewe hicho kiti umuachie professor |
|
Nisamehe kama nakosea maana mimi sio mwanasiasa |
|
Claps claps claps |
|
By... Mwl... Julius Kambarage Nyerere |
|
Kwa hiyo kitu kimoja tunataka kuelewa... |
|
Ni hali ya matatizo ya nchi yetu yalivyo sasa hivi... Eee!! |
|
Kwasababu... sera ya... ay... awamu ya kwanza... awamu yangu mimi... |
|
Imefanya mema... imefanya ya kijinga... |
|
Ya kijinga yanaachwa...!! lazima yaachwe... |
|
Ubaya wenu ni kwamba... mnaacha mema... mnachukua ya kijinga |