Nawaza kwanini sikumjuaga zamani (Oh mama) Pendo lake zito mpaka lavunja mizani (Oh mama) Yeye na mimi Kajol Sharukh Khani (Oh mama) Wasojua mapenzi pole jamani Nijali kuwa Bachelor, aibu gani! Aliyeumba dunia Akayaumba na mapenzi Wala hakukosea Ila mwenzenu mi siwezi Nilishapenda Ila nkatendwa Moyo ulidunda, masikini roho Mbona nlikonda Licha ya kuhonga Kuweka vibanda Nishaomba poo Mwenzangu bado hujajua Baki unicheke Kwako yamechanua Ngoja yanyauke Andazi si kitumbua, acha mapepe Ukipendwa tanua, kwanini nsideke? Jamani nimependa mie, nimependa mi Nimependa mi, nataka nimuweke ndani Mwenzako nimetendwa mie, nimetendwa mie Nimetendwa mie, mapenzi siyatamani Jama nimependa mie Nimependa mie Nimependa mie, nataka nimuweke ndani Mwenzako nimetendwa mie, nimetendwa mie Nimetendwa mie, Mapenzi siyatamani Ana mapenzi ya bara kachanganya na pwani Vipi nitajinasua? Rangi kama chotara, shape sio mjapani Marashi huzibi pua Ameumbika sina budi nisifie Akipika natamani nilipie Sehemu ya upanga uliweka kiwembe Ndo maana Mwasi akaona ajichenge Kwa wenzako sikia, sikia mwana Ila kwako utalia, utalia sana Mi nilikuwaga fundi, fundi zaidi yako Power ka milundi, nikiganda kama sumako Na kutia pesa madegeje, asiniache Nikamchanganya akolee, asiwake Penzi upepo wa bahari, mara kusi shwari Yaki-change hatari, na usiombe Jamani nimependa mi, nimependa mi Nimependa mi, nataka nimuweke ndani Mwenzako nimetendwa mie, nimetendwa mie Nimetendwa mie, mapenzi siyatamani Nimetendwa eh Mwenzenu ninatendwa Nimetendwa Nimependa mi, nimependa mi Nimependa mi, nimependa mi Nimetendwa mie, nimetendwa mie Nimetendwa mie, nimetendwa mie